Tuesday, April 12, 2011

ICC - Ukoloni umerudi


Mahakama ya kimataifa (ICC) ilianzishwa mwaka 2002, makao yake makuu yakiwa huko udachi katika mji wa Hague. Nchi nyingi duniani zimepitisha sheria za kuridhia kuanzishwa kwa mahakama hiyo, huku zikiahidi kuheshimu taratibu na maamuzi yake. Marekani, mwaka wa tisa tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo, bado haijaridhia! Nchi nyingine ambazo bado kutia saini ni pamoja na Israel na Sudan

Mahakama hii inapaswa kuingilia au kujihusisha pale panapokuwa na uhalifu wa kibinadamu ambao aidha serikali ya nchi au taasisi zake zimehusika, au nchi hiyo haitaki au haina uwezo wa kushughulikia uhalifu huo kisheria na kwa haki.

Tangu kuanzishwa kwake mahakama hii imekuwa kama ni ya Afrika. Kesi nyingi zilizopo huko ni kutoka Afrika, japo matatizo ya kuanzishwa kwake yapo katika mabara karibu yote.

Takwimu ya kesi za ICC


Takwimu kuhusu kesi zilizopo na zilizoisha huko Hague. Ramani ya Afrika karibu inajaa! huku mabara mengine hayajaguswa.


Mwezi huu tumeshuhudia wananchi 6 wa Kenya, tena wengine viongozi wakubwa wa serikali, wakipanda kizimbani huko Hague kwa kesi ya kuchochea fujo wakati wa uchaguzi mikuu uliofanyika mwaka 2007.

Swali ninalojiuliza ni kwamba, kwa nini serikali zetu za Afrika zinashindwa kuwawajibisha watu wake mpaka tuingiliwe na mataifa ya nje? Kumshitaki waziri mkuu msaidizi Uhuru Kenyatta ulaya wakati Kenya kuna mahakama na majaji waliobobea si ukoloni huu? Kuna tofauti gani ya haya na wakoloni waliokua wanawanyonga hadharani viongozi wetu waliowapinga.

Je, ukoloni umerudi?

Wasalaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...