Tuesday, April 12, 2011

Loliondo



Umati wa watu wakienda Loliondo
Kwa muda sasa magazeti mengi ya hapa nchini yameipa umuhimi mkubwa habari ya mchungaji mstaafu wa kanisa la KKKT anayeishi Loliondo mkoani Arusha. Mchungaji huyu inasemekana anatoa dawa yenye kutibu maradhi mbalimbali, ikiwemo UKIMWI.
Serikali kama kawaida yake imechelewa ku act. Baada ya habari kusambaa sana, maelfu ya watu kumiminika katika mji huo kwa matumaini ya kupata tiba, ndipo serikali imetoa tamko na kusitisha huduma ya mchungaji huyu.

Kwa ninavyojua mimi, serikali ina watendaji wake kuanzia kwenye kata. Kwa kuwa huyu mchungaji alianza kazi yake mwaka jana katikati (kama sikosei) watendaji hawa wa serikali walikuwa wapi? Mabwana Afya, maafisa wa serikali ya mtaa, kata, wilaya hata mkoa. Kama taarifa ilitoka chini kwenda juu, ilikwama wapi.
Haiwezekani serikali isubiri mpaka maelfu ya wananchi wake wameshakunywa dawa isiyothibitishwa na bodi ya madawa (TFDA) ndio wasitishe. Je kama ina madhara??
Wasalaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...